PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

MAPARACHICHI YA TANZANIA, YAWA LULU ULAYA

Image result for Maparachichi Tanzania


Soko kubwa na bei nzuri ya Parachichi imeimarika Nchi za Ulaya  za  Denmark, Ufaransa, Uholanzi, Norway, Hispania na Uingereza,* likitoa fursa mpya ya ustawi wa  zao hili kwa Watanzania, imebainika  kwamba *Parachichi la Tanzania limechukua chati ya Ubora katika Soko hilo.*

Uchunguzi kitakwimu una baini Mwaka 2012, kiasi cha mauzo ya nje ya Parachichi yalikuwa *kilo 488,492* tu, Miaka mitatu baadae Mwaka 2015 Tanzania *ilisafirisha Kilo 2,579,976 Ikiwa ni ongezeko la 428.48%.*

Kwa mujibu wa Kampuni ya Africado ambayo ni  kampuni ya kwanza ya Tanzania inayosafirisha Parachichi nchini Uingereza ambako maduka makubwa vyakula ya Ocado, Sainsbury, Tesco na Waitrose, *Parachichi la Tanzania linatajwa kuwa Bora zaidi katika soko hilo la Ulaya.*

*Walaji wa Ulaya wamenogewa na Parachichi linalozalishwa Mufindi na Kilolo* likitajwa kupatikana msimu ambao Nchi zaidi ya kumi zinazozalisha tunda hili kuwa Nje ya msimu wa uvunaji wa zao hili.

Parachichi linazalishwa na nchi zaidi ya kumi duniani  zikiwemo Argentina, Brazil, Chile, Colombia, Dominican Republic, Israel, Kenya, Mexico, Morocco, Peru, South Africa, Spain, Swaziland, Tanzania

Zao la Parachichi limeonyesha mwenendo mzuri wa bei na soko kubwa Ulaya parachichi moja likiuzwa kwa hadi *Shilingi za Kitanzania 7000/- ama Paundi 1.95 hii leo, fulsa hii inaangukia Tanzania.*

Kipindi cha mavuno cha sasa ni Juni hadi Agosti, huku Tanzania pekee inaweza kuvuna na kusambaza kuanzia mwezi Machi hadi Oktoba mwaka kila mwaka.

Sisi kama Taifa ni muda sasa wa kuacha mambo yasiyo ya msingi na kujikita na fursa kubwa kama hii.
Sasa kwa uhakika kabisa, tujikite katika kilimo na hasa kunapojitokeza fursa ya soko kubwa la mazao kama lilivyo parachichi kwa soko la Ulaya wakati huu.

Kwa sasa wanaonufaika zaidi na soko hili ni wawekezaji wageni walioshtukia mapema fulsa hii.

Nchi yetu... inafursa nyingi zitakazoleta
*Matokeo chanyA+* kiuchumi


Mche mmoja wa mparachichi unaweka matunda 3000 na heka moja inachukua miche 109 sasa zidisha 109 × 3000 =327000 

Parachichi moja kutoka Tanzania kwenye Supermarket Uingereza ni Paundi 1.95 sawa na shilingi 7000 sasa nambie Mkulima wa Tanzania auze parachichi moja shilingi 3000 tu kwa parachichi za heka moja 327000 sawa na shilingi ngapi wale watalaam wa Hesabu......

Salamu hizi zimfikie waziri wa kilimo na waziri wa viwanda Uwekezaji na Biashara Tanzania........

kilimo ni Biashara ni wakati Muafaka sasa Tanzania kuanziasha kampeini ya kila kijana nchi Nzima kuwa na Heka moja ya Kilimo kuelekea Uchumi wa  Viwanda Tanzania.....

No comments