# KUTUMAINI NI ZAIDI YA KUAMINI # by King Chavala
Shalom!
Imani ni Uhakika wa mambo yatarajiwayo
Tumaini ni Mategemeo ya uhakika kwa hayo mambo yatarajiwayo!
Unaweza kuamini jambo fulani kutokea,lakini ukamtumainia msababishaji wa jambo!
Labda niseme namna hii...Unaweza kuamini kuwa Utanunua gari, Lakini Ukatumaini Mshahara wa kazi unayofanya ama faida ya biashara fulani!
Imani ni Jina ila Tumaini ni tendo-jina!
Kuamini peke yake hakutoshi, ila kutembea katika kile unakiamini pasipo shaka huku ukitarajia kile kisichoonekana!
Wewe unasema unamwamini Mungu,Hongera sana! Lakini unafikiri kuamini peke yake kwafaa kitu??
Yakobo 2:19
Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
Nafikiri sasa umeona kuwa hata mashetani Wanaamini na kutetemeka ila hawamtumaini Mungu!
Tumaini huendana na UTII, na kimsingi huwezi kukitii kitu ambacho hukijui kwa kina! Kwahiyo imekupasa KUMJUA SANA MUNGU, na hapo utakuwa unaweza kuwaza,kufikiri na kuamua kwa muono wake!!
Shadrack, Meshack na Abeidnego walipotishwa kuwa watatupwa kwenye tanuru la moto,baada ya kutosujudia sanamu mara ya kwanza, na Mafalme akasema Ngoja tuone mara hii nani hasujudu...Wakamwambia wala usisumbuke,maana HATUWEZI KUSUJUDIA SANAMU!, MUNGU wetu atatuokoka na vyote, lakini hata kama asipotuokoa,bado hatuwezi kusujudia!!
Yaani kwa lugha rahisi ni kuwa Mahusiano yetu na yeye hayawezi kuvunjwa na chochote, Sasa hiyo sio imani,ni Tuamini!
Unaweza ukawa na Imani na Ujuzi na Maarifa yako,lakini Wa Kutumainiwa ni Mungu tu!
Ziamini akili zako na Mipango yako,lakini Mtumaini Mungu!!
Bilionea akiwa juu, hana tu imani na mikono yangu,ila Anatumaini kabisa kuwa siwezi mwacha aanguke na ndio maana unaona ANACHEKA SANA; Na Malkia wangu,japo anapata hofu na imani inaweza kuingiwa na mushkeli juu ya mrusho huu wa raha,Lakini Analo tumaini kuwa Baba hawezi mtupa Mwanae!
Lakini hata Mimi ninaona raha sana!
Na Mungu anatamani tumtumaini, sio kwasababu ya chochote alichotupa au tunachotarajia,ila kwasababu Tunamjua na Tunayo hakika kuwa Anatupenda
LEARN TO TRUST GOD!!
# Nakuonya hii usijaribu, maana unaweza ukamrusha na kumbe Ndio saa ya Unyakuo hahah!
~Walk Straight, Live Well ~
No comments