PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

"FURAHA YAKO ISIWE KIPAUMBELE CHAKO, ILA MAPENZI YA MUNGU YAWE KIPAUMBELE CHAKO "



"-Leo tunapokuwa tunapokuwa tunaangalia tulikojikwaa hasa kwa wazazi wetu akina Adamu, kama si kwamba walitanguliza 'interest '-zao mbele badala ya "interest "-za Mungu, yumkini tusingelikuwa hapa tulipo leo! Neno la Mungu, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote kwa akili zako zote kwa nguvu zako zote.  ..Matokeo mengi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, ndoa zilizovunjika, mafarakano ktk ndoa, mauaji ya kikatili, utapiamlo, nk ni matokeo ya kila mtu kuweka 'interest "-zake mbele kuliko za Mungu na kuweka za mwenzake pembeni kabisa! Ikiwa, tunapaswa kunyenyekea ktk mapenzi yote ya Mungu ni wazi ya kuwa, kama tungelikuwa Jehanum, tusingelikuwa nã uchaguzi zaidi ya kwamba, tungetii bila shuruti ili tuungue! 
Kwa maneno mengine ikiwa wataokwenda Jehanum watakuwa wanatii kinachowapata ni kumaanisha walitumia hiari yao vibaya walipokuwa hai kwa kuweka 'interest '-zao mbele kuliko mapenzi ya Mungu! Maana yake hata sasa tunaweza kujiweka chini ya mapenzi yote ya Mungu! Hatuna budi kujinyenyekeza ktk mapenzi yote ya Mungu SASA na kutaka kwa maombi ya dhati ili tutembee naye maadamu bado ni mchana! Yak 4:7-.Azimia kumwishia Mungu! (Kyombo Phanuel Paul -Dar).

No comments