PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News


UKISHINDWA KUPENDA WEWE NI MTUMWA

Katika mambo ambayo ni utumwa na mateso ni pale mtu anaposhindwa kupenda. Ni utumwa usioelezeka kama huwezi kupenda. Ni mara nyingi nasikia watu wanasema sitopenda tena, ooh siwezi penda kama nilivyompenda yule, nilijitahidi kupenda lakini nimeshindwa..na nyingine nyingi. Lakini ukijiona unaongea hizo.sentensi ujue ushaanza kuwa mtumwa au ni mtumwa tayari katika kutokupenda.
Sisemi hivi kwa sababu sijawahi umizwa na kupenda au kuumia sababu ya kupenda hasha nasema hivi sababu katika vitu mwanadamu ili aishi kwa kufurahia maisha ni kupenda. Nawaza tu pamoja na madhambi na makosa na uovu mwanadamu alifanya na anafanya kwa Mungu bado huyu Mungu anatupenda. Unajua nakupenda, nakupenda sio kwasababu una umbo na sura ya kuvutia sana. Nakupenda sio kwasababu unapesa na mali nyingi, nakupenda sio kwasababu nilikosa msichana/mvulana wa kumwambia nakupenda. Nakupenda sio kwasababu wengine wanapenda hasha. Bali nakupenda kwasababu ni raha kukupenda, nakupenda kwasababu kupenda sio utumwa. Nakupenda kwasababu Mungu amenipa wewe nikupende. Nakupenda kwasababu nimechagua kukupenda wewe na sio mwengine. Nakupenda sababu nakupenda. Inawezekana kabisa kuna wakati nilikosea au nakosea lakini unajua kuwa nakupenda. Upendo usio kinafiki huwa haufichiki wala hauna hila ndani yake. Upendo wa kweli hauhangaiki kusema sitopenda tena kwasababu mwanadamu ni asili ya upendo. Najua upendo wa kweli huanzia ndani na kuchomaza nje kwa njia ya matendo. Ni kazi sana kuulezea upendo wa kweli. Ni ngumu kupata neno moja litakalotoa maana ya neno nakupenda. Lakini matunda ya upendo kamwe huwa hayafichiki kwa apendwaye. Kwako upendwaye nami. JIFUNZE KUJIFUNZA KWA HISANI YA WAPENDAO KUPENDA. Mwl Makwaya Kuwa ni Kufanya.

No comments