PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

MTAKATIFU MALAYA!



Ndio mtakatifu malaya na sio malaya mtakatifu. Ni sawa na chips kuku ni tofauti na kuku chipsi. Au wali samaki ni tofauti kabisa na samaki wali. Kilicho kingi ndicho kinashikilia jina. Ndio kisa cha mimi kuandika mtakatifu malaya, nikiwa na maana utakatifu ndio unaonekana sana machoni pa watu wengi na sio umalaya unaoonekana na watu wachache pamoja na wewe mwenyewe. Yeah nimesema mtakatifu malaya kwa kuwa wengi wanaweza kukutetea hadharani juu ya utakatifu wako ila wachache sana pamoja na wewe wataishia kuguna na kunyamaza kimya. Burudani ni pale wazee wetu wanapoonaga malaya ni mtakatifu na mtakatifu ni malaya halafu wanatoa na hoja kabisa. Kuna wakati wala siwashangai wazee na wachungaji kutokuwa na imani na kizazi chetu ila ashukuriwe Mungu kupitia Yesu Kristo ana imani kubwa na kizazi hiki ndio sababu akafa msalabani.

Kuna watu wanapenda kuwa watakatifu malaya. Kwa makusudi kabisa wamechagua kuwa hivyo na wanafurahia na wanaona ni jambo la kawaida. Sio kwamba hawajui wanachokifanya ila wanajua na kupenda wanachokifanya. Wanajifanya hawajui Kuwa ni heri kuwa baridi au moto kuliko kuwa katikati. Yaani ni heri kuwa Mtakatifu au kuwa malaya kuliko kuwa mtakatifu malaya. 

"Nayajua matendo yako, ya Kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

Basi, kwasababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu."
             Ufunuo 3:15-16

Sasa wale wanaojua kabisa ni nini wanafanya ni rahisi sana kukuta wanalugha ya kujitetea katika wanayofanya. Hawapendi kuonywa wala kuambiwa ukweli. Wanasahau ukweli usioupenda ni ukweli pia. Wengi wao hawana hata nia ya kutubu maana umaarufu umekuwa na nguvu kwao kuliko ukweli. Wanafurahia kwasababu kuna wengi wanafurahia pamoja nao katika udharimu wanaofanya na utaishia kuwasikia hakuna mwanadamu mkamilifu. Kujitetea kwingi kuliko kukubali kwamba wanakosea. 

"Ukiona kila ukiambiwa ukweli unakimbilia kusema mbona fulani anafanya na ni mtumishi mkubwa kabisa, basi ujue tu, utakuwa unapenda kuwa mtakatifu malaya kuliko kuwa mtakatifu au kuwa malaya"

#Ukweli usioupenda ni ukweli pia#

FIKICHA AKILI

Mwl Makwaya 
Kuwa Ni Kufanya.

Ukiwa kwenye kundi hili kuishi maisha ya maigizo ni jambo la kawaida sana na unaweza kuwa umewazidi wale wa Hollywood au Bollywood au Nollywood kwa namna ulivyo msanii au muigizaji mzuri. Na hivi watu wengi hushindwa kutofautisha hisia na upako basi ndio inakufanya uamini uko juu. Kama ni mahubiri utahubiri kwa namna watu watasisimuka tu, kama ni kufundisha utafundisha kwa jinsi watu watahemuka tu na kama ni kuimba utaimba kwa namna watu wataona huzuni na kutoa machozi na kuishia kusema hakika leo tumemuona Mungu. 

Lakini pia kuna kundi la pili la watakatifu malaya. Hili ni lile kundi hawapendi kabisa kuwa mtakatifu malaya. Ila kila wakijitahidi waache umalaya wanashindwa. Wengine imefikia hatua wanajichukia maana hawaipendi hiyo hali. Hawa wanatafuta namna ya kutoka kwenye utakatifu malaya kwa nguvu zao na bado wameshindwa. Kile ambacho hawataki kukifanya ndicho wanakifanya na kuishia kuumia. Tofauti ya hawa na wale wa kwanza ni kwamba wale wa kwanza wao wanafurahi kuwa mtakatifu malaya ila hawa wapili hawafurahii na wako tayari kuacha ila wanaachaje sasa.

"19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.

20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

21 Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.

22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,

23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.

24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi."
                 Warumi 7:19-25

Paulo naye alikutana na hali hii. Yale asiyopenda Kufanya ndiyo anafanya. Na anayopenda kufanya hayafanyi. Ila anamalizia kwa jambo moja zuri anamshukuru Mungu kwa Yesu maana kupitia yeye inawezekana kabisa kutoka kwenye utakatifu malaya. 
Mungu anaweza kukutoa huko kama umedhamiria na unataka kutoka huko.

Mungu anapotuita kwa mwana wa pendo lake huwa anatubadilisha na kutufanya viumbe vipya. Anahangaika na kubadilisha fikra zetu. Anahangaika kututakasa kila iitwavyo leo. Ila anashida na wale wenye kiu, wale wenye shauku ya kubadilika na sio kujibadilisha. Na wala haangaiki na wale wanaojiona wana sifa bali wale wanajua kabisa hawana sifa ila wanaamini katika Mungu basi huwapa sifa na kuwafanya tofauti. 

Sijajua upo kundi lipi kati ya hayo mawili ila jambo moja ninauhakika nalo Mungu anakupenda na hapendi ubaki katika MTAKATIFU MALAYA. Anaweza kukutoa huko na ndicho kilichomfanya akubali kufa msalabani. 

MALAYA - Inaweza Kuwa ni lugha picha tu.

#PENDO HUBADILISHA#

JIULIZE KWA UPOLE

Mwl Makwaya 
Kuwa Ni Kufanya.

No comments