PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

MI SIJAWAHI PATA CHANGAMOTO..

Image result for changamoto

Ndugu mmoja akaniambia brother Mimi katika maisha yangu kitu nisichokipenda ni Changamoto,Ndiyo Maana hata sijawahi pata,yote kwa kuwa sizipendi,nikamuuliza wewe una muda gani Duniani akaniambia miaka 27,nikamshangaa sana,nikahisi siyo Binadamu,kumbe kuna Asili ya Familia zinalea watoto katika kuwaaminisha kuwa kila Siku na wakati ni sahihi na sawa,kila hali nzuri asili yake ni nzuri,nikamuuliza tena kwani wewe Changamoto unajua ni nini? Akajibu Kupingwa,kikwazo,tena akasema sijawahi kutana na kikwazo chichote Tangu nizaliwe,!!!Ooohuu!!

Yawezekana na wewe unajivuna na kujidai hukutani na Changamoto mpendwa,yawezekana na wewe ni MTU uliyekuta kila mazingira sawa,yakakupumbaza uone kuwa Changamoto zipo kwa baadhi hapa Duniani,NO,Ukiona hujakutana na Changamoto yoyote duniani yangu uzaliwe,UKAPIMWE AKILI,samahani kwa kauli ngumu ila ni kweli AKILI yako haiwezi kuwa Sawa na utakuwa na Maisha Magumu ajabu sana,utaishi kwa taabu mpaka utajua kutozaliwa ni bora,,Ukiona Unaishi Siku moja au mbili hujapata Changamoto yoyote kifamikia,kiuchumi,kikazi,kiofisi na ndoa ujue UMEPUNGUZA uwezo wako mkubwa sana wa kutatua Changamoto nyingine,au ujue utakuwa butu sana,hivyo Anayekutanana Changamoto nyingi Yuko Imara zaidi kimapambano kuliko wewe...Mtoto wa mtaani Yuki Imara sana ktk kupambana na Vita maisha,mfano ukamfundisha thamani ya maisha yake huyo,Ni itakuwa hashikiki tena.

Changamoto hunoa na kuimarisha,kama hukutani NAZO ujue wewe ni Dhaifu Akili,Fikra mpaka Mwili,Hujapata Changamoto Sikitika,Usifurahi Maana Changamoto ndio Mwasisi wa Ushujaa na Ushindi.



0762490145.

No comments