#UNAYEOA/OLEWA NAE ANA HIKI...
Jambo kubwa unahitaji kujua ni kwamba MTU unayetaka kumuoa au kuolewa nae amefungiwa catalyst (Kichochezi) Ndani yake cha kukusaidia kufanikiwa au kukufanya ufeli katika maisha yako,kuna watu ambao kabla hawajaoa au olewa walikua wanapata pesa nzuri sana,walikuwa wanaheshima na kuheshimika sana,walikuwa wanabusara sana,na maadili yao yalionekana vizuri mbele za Mungu,na baadhi ya watu,lakini Mara baada ya kuolewa/kuoa hawapati tena Mafanikio kama Yale,,milango ya fikra imekuwa mizito na wameshindwa kuungana kujenga yale ya awali..Kuna wengine kabla ya kuoa/olewa walikuwa na uchumi wa kawaida sana,walikuwa hawana kazi,walikuwa hawajali ni maisha gani wanaishi ya kukubalika au lah,,ya kujaliana na Ya maadili sahihi au lah,Hawakujali,Lakini Mara baada ya kuoa/olewa,Wameshuhudia kuongezeka kwa msukumo chanya,kujua thamani na uchumi kuimarika,wengine wakapata kazi, wakaimarika kijamii na ushikiano na watu kukawa Chanya zaidi..
Hivyo yawezekana kuna vitu haviendi kama ulivyodhani,na kutarajia na ulivyohitaji,Sio kwamba huwezi hapana ni kwamba Mchochezi hayupo,hujaoa/olewa.Yawezekana Fikra zako bado zipo tied(zimejibinafsisha) kwako,kumbe zilitakiwa kuchangiwa,umekosa mhemuko wa nguvu ambao udhaifu huo yupo wa kuweka sawa naye sio kila MTU hapana,sio yeyote yule hapana ni Mmoja tu Mke/mume wako...Hivyo usitake kujiaminisha kuwa kila MWANAUME anayevaa suruali,au kila suruali unayoiona inaweza kuwa ya Mume wako,Au kila sketi iaweza kuwa ya mke wako Hapana,Hata wewe unaweza vaa sketi/suruali,.Kuna mambo hayataenda wala hutayafanya Mpaka Umeoa/olewa na sio kila unayemdhani ni sahihi,sio kila unayemtaka ndiye Hapana, Bali unayemhitaji,Maana ni CATALYST (Mchochezi),Anaweza kukuchochea ukapanda juu na kufanikiwa sana au akakuchochea ukashuka chini na kupotea kabisa,#INGIAVIZURI.
With My Workmate,#Judith,I salute you.
#TETE,#MotivationalSpeaker. Sadicktete24@gmail.com .0762490145,
No comments