PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

Katongo Wisdom


Hatua ya tatu kwenye mzunguko wa biashara/taasisi (organization life cycle )... tunaiita GO---- GO STAGE .

Hii ni hatua ambayo biashara imeshatambulika vizuri na inafanya vizuri sokoni kwa maana ya mauzo na kuongeza wateja; lakini ðŸ¤”🤔!! Shida iliyopo ni kwamba ...mchezo wote huo unafanywa na mtu mmoja (one man show )...

Mara nyingi mmiliki wa biashara hapa anajiona yeye ndo Genius   na hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kumshauri kwani matokeo ya ukuaji wa biashara yanamfanya kuwa kipofu wa hali ya soko ya siku zijazo. 

Hatua hii ni ngumu sana kuvuka kwani inahitaji mmiliki (owner) kukubali mabadiliko ya kiuongozi na kimfumo ili taasisi iweze kuwa imara zaidi na kuongozwa kwa mifumo na uongozi unaoweza kuhakikisha maendeleo ya biashara ni ya kudumu (going concern ) hata kama patatokea kifo cha mwanzilishi wa biashara husika. 

Kwenye hatua hii , mmiliki wa biashara anashauriwa kufanya yafuatayo;

✔Kutengeneza mifumo thabiti ya kuongoza biashara ili kuhakikisha biashara inajitegemea kwa asilimia 100.

✔Kuruhusu mabadiliko ya kiuongozi kwenye biashara ili kuleta maboresho na kukuza biashara kwa kiwango cha hali ya juu. Mwanzilishi hapa anaweza akabakia kuwa sehemu ya uangalizi (overseeing the management )...uangalizi wa biashara lakini akauachia uongozi kupeleka gurudumu. 


Itaendelea 

#Killingpoverty 
#Mylifemyresponsibility 

#Internationalmc 
#mckatongo 
#mbaEsami 
#Katongobusinessconsultant 

No comments