PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

MAMA ALINIAMBIA KUPITIA MAHARAGE




Nilipokuwa mdogo nilikuwa namuona MAMA akichambua maharage, alikuwa anaweka *maharage mazima*  kwenye sufuria ya kupikia, na *maharage mabovu* alikuwa anayatoa kisha anayatupa mbali jalalani.!

Cha kushangaza.. mvua ikinyesha maharage yale yale mabovu ndio yanakuwa ya kwanza kuota na kuchepua..
Yalitupwa yakiwa mabovu yasiyofaa.. lakini yanaota.. kisha yanatoa maharage mengine mazima na bora zaidi kuliko yalivyotupwa mwanzo yakiwa mabovu.!

Hii imenifanya nijifunze kuwa ni muda/wakati tu utakao amua hatma yako.. Pia jinsi Mungu anavyokuaona ni tofauti kabisa na watu wanavyokuona..
Inawezekana ukaonwa/ukajiona kama maharage mabovu leo.. lakini hakika *mvua ya Mungu* ikikunyeshea UTAOTA na kuwa wa thamani na KUZAA/KUTENGENEZA WATU WENGINE BORA ZAIDI YA WEWE..

Inahitaji wakati tuu
Uvumilivu..
Na kujua kusudi la Mungu na mawazo ya Mungu ni tofauti na yawanadamu..

USIKATE TAMAA WALA USIVUNJIKE MOYO
YOUR RAIN SEASON IS COMING
Wewe ni bora na unafaa sana.!
Kila jambo chini ya jua lina wakati wake haijalishi jinsi ulivyo leo.

No comments