UJUMBE WA KWARESIMA KWA WOTE
Kwa tafsiri isiyo rasmi sana.
Kuna kanisa lililokuwa limechakaa sana katika Kijiji kimojawapo huko Brazil,hata kuta zilitaka kuanguka.
Baada ya ibada ya misa Padre aliwataka waumini kama wanaweza kujipanga na kujihamasisha wafanye harambee kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.
Aliwaambia wanaweza kuchangia chochote kulingana na jinsi Mungu anavyowakirimia.
Kama una pesa leta,kama unauza nyanya leta zitapigwa mnada na hela itakayopatikana itabust mnada, hivyo hivyo kama unauza hardware ni vema zaidi,unaweza kuleta hata misumari,mabati kwa sababu tutaezekea.Chochote mnaweza leta tufanye mnada.
Basi siku ya harambee ilipofika waumini walikuja kwa wingi sana, baadhi walileta fedha,wengine vitu mbalimbali kulingana na aina za kazi wanazozifanya. Katika hali hiyo waliona jambo geni sana ambapo hawakutarajia kuwepo katika mnada huo.
Muumini mmoja alileta geneza akaliweka mlangoni mwa kanisa jambo lililoleta tafrani miongoni mwa waumini na kuulizana nani kafa na inawezekanaje kuwepo na ibada ya mazishi siku ya jumapili?
Watu walianza kuulizana nini maana yake na walianza kumnyooshea kidole Mzee mmoja aliyekuwa amekaa kona moja ndani ya kanisa hilo kukuu.Alikuwa ni mchonga majeneza,baadhi ya waumini walimtazama kwa macho ya ukali lakini yeye hakujali,kwani alizingatia aliyosema Padre kwamba kila mtu alete kile ambacho Mungu alimbariki. Kwahiyo yeye alileta jeneza ambayo kimsingi ndio kazi ya mikono yake.
Baada ya ibada kwisha mnada ulianza. Waliokuwa na fedha,hardware materials,nyanya n.k waliweka vikapigiwa mnada na pesa zilipatikana. Mwishowe mchonga majeneza alipeleka jeneza lake mbele ya kanisa na kusimama. Waumini wote walikaa kimya, hata ungedondosha pini ingesikika!
Mzee alitoa ofa ya Tsh 15,000 akasema namnunulia Padre jeneza.
Padre akahamaki kwa mshtuko mkubwa,haraka naye akatoa 20,000 akasema namnunulia kiongozi wa WAWATA.
Mama naye akapaniki,nasema hapana hapana hili siyo jeneza langu...! Akamnunulia Katekista kwa 30,000!
Katekista kwa hasira akamkoromea mama na kumwambia unataka kuniua?Harambee iliendelea.Ukweli hakuna aliyetaka kununuliwa jeneza na mwishowake babu mmoja tajiri alimnunulia yule mchonga majeneza kwa 100,000.
NYONGA jeneza alilibeba jeneza lake akicheka kuelekea dukani kwake.
Muuza majeneza ni mtu anayepata riziki yake kutokana na misiba lakini aliweza kuchangia harambee kubwa kuliko watu wote na bila kutoa hata senti moja kutoka mfukoni mwake!
FUNDISHO
Unaweza kumtumikia Mungu kwa njia mbalimbali.
Labda watu wanaweza kukuchukulia poa tu na ukajiona sii lolote. ..Lakini Mungu anataka umtumikie kwa nafasi na level ulionayo na atakuinua.
Tafakari............
Nakutakia kwaresma njema.
No comments