MAISHA NI HAYAHAYA!!!
Ni kauli ambayo huenda hata wewe ni mmoja wa watamkaji na waamini wake,kauli hii imetumika sababu ya wengi kuzoea Maisha, imekuwa sababu ya walio wengi kuhairisha kufikia ndoto zao bila kujua,imewafanya wengi kukata tamaa,na wakati mwingine ikawafanya wengi zaidi kuamini kuwa hawawezi kwenda mbali zaidi ya pale walipo,hivyo wanaona waendelee kusukuma siku tuu maana kufanikiwa zaidi haitowezekana kwa imani yao,na kusema MAISHA NI HAYAHAYA.
Pia marafiki wametumika kutushia wenzao wanapokuwa wanapambana na ndoto zao,hivyo Wanaambiwa MAISHA NDIYO HAYAHAYA hata ukipambana vipi kutoka ni majariwa,usijifanye unajua kuwa busy sana,MAISHA NI HAYAHAYA, ni kauli ya vitisho sana kwa usiye na msimamo wa FIKRA,na KUJITAMBUA, lakini pia kauli hii imekuwa chanzo cha Nidhamu mbaya sana ya Fedha,ambapo wakutanapo marafiki wawili wanatumia fedha pasi kufuata mipango yao,na kusema MAISHA NI HAYAHAYA. Lazima uwe Makini na maisha yako,mtazamo wako,Focus(Mwelekeo) wako, Nia,na Fikra zako,Hivyo Lazima Ujiamini na nidhamu yako,ANGALIA sana MARAFIKI ulio nao,chunga Zaidi MANENO YA KINYWA CHAKO,maana huwa yana nguvu ya kuhuisha au kuua nguvu ya kufanikiwa kwako,.....
#TETE,#MotivationalSpeaker.
No comments