UKUBWA WA CHANGAMOTO NI KISHINDO CHA MAFANIKIO!
UKUBWA WA CHANGAMOTO
NI KISHINDO CHA MAFANIKIO!
Tembo na mbwa
walishika mimba kwa wakati mmoja. miezi mitatu baadae mbwa alizaa watoto
sita.
Baada ya miezi sita
mbwa alibeba tena mimba nyingine, na ilipofika miezi tisa alizaa watoto wengine
kumi na wawili
Miezi kumi na nane
baadae mbwa aliamua kumfuata tembo na kumuuliza "unahakika kwamba kweli
una mimba"? Maana sote tulibeba mimba wakati mmoja, mm nimesha zaa mara
mbili mpaka sasa nina watoto zaidi ya dazani lakin ww bado una mimba ileile tu,
nn kinaendelea?
Tembo akajibu
"kitu kimoja ambacho inakupasa utambue ni kwamba nilie mbeba tumboni
mwangu sio mbwa bali ni tembo. AkaendeIea huku akisema ninazaa mara moja tu
ndani ya miaka miwili, lakin siku nikimshusha mwanagu ardhini dunia
lazima ihisi kitu, na pindi mwanangu anapokatiza barabarani,binadam husimama na
kusitisha shughul zao hivyo bas nilicho beba kina thamani kubwa sana."
FUNZO
Usipoteze imani yako
unapoona watu wengine wanajibiwa maombi yao, wala usivunjike moyo kama bado
hujapokea baraka zako toka kwa Mungu.
Sema na moyo wako
kwamba"siku yangu ya kupokea baraka zangu inakuja, Amini mola hachelewi
wala hakawii, punde mola atajibu maombi yako na kwa hakika utaishangaza
dunia."
MKULIMA Omba na Fanya
kwa vitendo bila kukoma KISHINDO CHA TEMBO KIPO NJIANI
No comments