PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

JPM: Sikutaka fedheha, atoa zawadi ya karne kwa Taifa Stars

RAIS John Magufuli amekutana na Timu ya Soka ya Taifa-Taifa Stars- leo tarehe 25 Machi 2019 ambapo amewaeleza, alishindwa kwenda uwanjani kuangalia mechi kwa kuogopa fedheha. Anaripoti Bupe Mwakiteleko…(endelea).
“Niliogopa fedheha, niliamua kubaki hapa hapa nyumbani kuangualia mpira,” amewaambia wachezaji hao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Taifa Stars walioambatana na viongozi mbalimbali wa nchi, Shirikisho la Soka nchini (TFF) na wachezaji wa zamani waliosakilishwa na Peter Tino walialikwa na Rais Magufuli kwenye Ikula kula chakula cha mchana leo.
Akizungumzia mechi ya jana tarehe 24 Machi 2019 Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa na kiwango cha wachezaji wa Taifa Stars kwa kuonesha kiwango kikubwa.
Kwenye mchezo huo dhidi dhidi ya Uganda, Tanzania ilishinda 3-0 na hatimaye kufuzu michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Misri.
“.. Nimeamini kuwa, kumbe tunaweza lakini niliona baada ya kufunga moja na kutokana na Tanzania hii wanavyocheza, nikaamini goli litarudi sasa hivi. Mke wangu akaniambia Tanzania leo tutashinda, nikamwambia wewe unajua nini?” amesema Rais Magufuli na kuongeza:
“Nilipoangalia kwenye televisheni zetu nikaona wachezaji wanasifiwa sifiwa nikaamua kubadilisha na kuweka Super Sport na huko nikaona wanawasifia, nikaona kweli wanacheza vizuri.”
Rais Magufuli amesema, baada ya Stars kushinda goli la tatu, alihamia kuangalia mechi ya Cape Vade na Lesotho kuangalia kama timu hiyo (Lesotho) imefungwa “kule nikaona bila bila.”
Katika ghafla hiyo ya chakula cha mchana na wachezaji pia uongozi wa TFF Rais Magufuli amesema, jana tarehe 24 Stars walimaliza machungu yake.
Kutokana na furaha hiyo, Rais Magufuli amemwagiza Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu kuhakikisha wachezaji hao wanapatiwa viwanja jijini Dodoma.
“Mimi nimeona niwape zawadi kidogo, sina kitu lakini kwa niaba ya Watanzania nimeamua kuwapa zawadi. Nimeamua kuwapa kila mmoja viwanja Dodoma. Tena itakuwa vizuri viwanja hivyo viwaka wapamoja,” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa, kama Taifa Stars itaendelea kucheza vizuri kama ilivyocheza na Uganda, inaweza kufika robo ama nusu fainali.
Amesisitiza kuwa, wachezaji hao kama wataendelea kucheza vizuri, wataonekana na watachukuliwa kwenda kucheza nje (mkiendelea kucheza hivyo wengi watachukuliwa. Hilo ndio ombi langu kwa kuwa mchezo ni biashara na biashara hii tusiilazie damu.”
Amesema, Wizara ya Michezo sasa anaweza kuzungumza nao vizuri . “Nataka waziri akiniambia tunashinda, tushinde kweli sio tushindwe. Nafuu anyamanze aseme bana hapa tunapigwa na haka katimu kadogo.”

No comments