PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

UKITAKA MTOTO WAKO AWE RAIS NI RAHISI.

MLEE MTOTO KATIKA NJIA IMPASAYO NAYE HATAIACHA HATA ATAKAPOKUWA MZEE Mithali 22:6



Ukitaka maisha yako na namna Mtoto wako awe inawezekana maana neno linasema tuwalee ipasavyo Mithali 22:6 inamanisha kuwa wewe ndio una nafasi ya kumfanya mtoto awe vile upendavyo lakini wazazi wameacha malezi kwa walimu na Dunia ambako huko mtoto huchakura kama kuku wa kienyeji Mungu wetu ni mwaminifu katupa kila nafasi ya sisi kuonyesha Nguvu ya uumbaji iliyoko ndani yetu maana tumumbwa kwa mfano wa Mungu ni wewe mzazi kuamua Mtoto awe nani nakuanza kumuweka katika mazingira hayo fikiria una mtoto unataka awe Rubani lakini hana Toi hata moja la Ndege hujampeleka hata uwanja wa Ndege hapo utakuwa humuandai kuwa kila unachokitaka.

Anza kubadilika na ungana na mtoto kufikia ndoto zake Hata kama wewe huna hiyo fani wala hakuna ndugu na Rafiki mwenye fani unayotaka mtoto wako awe anza kuhakikisha unatafuta connection hakika Mungu atajidhihirisha kupitia wewe mzazi maana hakuna aliyezaliwa kuwa Flani bali mazingira na msaada kutoka kwa Wazazi ni Muhimu pia ukitaka awe Rais anza kuandaa mazingira ya Kitawala ndani ya Huyo Mtoto

Elirehema Msuya
www.youtube.com/kingdombusinesstv


No comments