PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

UNAKULA NINI KIMWILI NIMUHIMU PIA UJUE KIROHO UNAKULA NINI?


Ili uwe na Afya Bora inahitaji uwe unajuwa pia Chakula Bora na si Bora Chakula watu wengi huwa wanaamua kwa kujuwa au kutokujua au kutokana na hali ya Maisha huangukia kula kila wanachokutana nacho, Sijasema hicho chakula kwenye picha kuwa sikizuri la Hasha ila nilimanisha ni vizuri ukachaguwa kula chakula chenye manufaa kwenye mwili wako maana Afya yako nimuhimu sana na nimatokeo ya vyakula unavyokula na asilimia nyingine utahitajika mazowezi.

Kiroho pia unatakiwa ulishe Roho yako Neno la Mungu maana unaweza ukapata Neno lisilokujenga kiroho kama inavyowezekana kuona mtu anaumwa ugonjwa wa kwasha koo ya kimwili vivyo hivyo unaweza ukawa na kwasha koo ya kiroho kwa sababu hukupata Neno la Mungu bali ulipata mafundisho yaliofikiriwa ni ya Mungu kama unavyotamani kuwa unakula chakula kizuri cha Kimwili basi amua kutafuta Neno sahihi la Mungu kwa Nguvu zote. Isaya 55:6

Elirehema Msuya
www.youtube.com/kingdombusinesstv
www.kingdombusinesstv.blogspot.com





No comments