PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

KANUNI YA KUFUNDISHIKA


Wengi tunatamani sana kufanikiwa lakini tuna tatizo  kubwa la KUTOKUFUNDISHIKA 
Kuna watu wengi tunao katika jamii wana tatizo kubwa sana la KUTOKUFUNDISHIKA 
Wanaona wanajua kila kitu kwasababu ya nafasi walizonazo, hela walizonazo, Biashara walizonazo, Ndoa walizonazo, familia walizotoka na kadhalika 
Na kwasababu ya KUTOKUFUNDISHIKA kuna mahali kwenye maisha yao kuna UKOMA hauondoki 
Unapokuwa mtu unayefundishika utakuwa mnyenyekevu kujifunza hata kwa watu walio chini kwako ambao wewe unaona ndio wanahitaji msaada wako.

Tunajifunza kwa Naaman katika 2 Wafalme 5, japo alikuwa; 
1. Jemadari wa vita
2. Mtu wa Mkubwa wa Kuheshimiwa 
3. Anayetembea kwa msafara wa magari na farasi 
ALIKUWA NA UKOMA
Inawezekana wewe ni binti mrembo, una kazi nzuri, una maisha mazuri, ni mfanyabiashara mkubwa, uko very smart darasani, una ndoa nzuri, lakini kuna mahali una ukoma 
Sijui ukoma wako ni upi
Labda ni ;
Ugonjwa 
Ndoa imekuwa ngumu 
Uchumi umekuwa mgumu 
Umekosa kibali kila unapoenda unakataliwa 
Biashara zako zimekufa 
Pole sana
Yakupasa kushuka na kunyenyekea kama Naaman na kuwasikiliza watu ambao wako chini yako maana wanajua penye msaada wako
Msichana au kijana wako wa kazi hapo nyumbani inawezekana anajua unapopatikana msaada wako, Yakupasa kushuka na kufundishika ili upate MUUJIZA wako
Usicheleweshe muujiza wako kwasababu ya Kiburi cha pesa ulizonazo, nafasi uliyonayo, Ukubwa ulionao, akili ulizonazo FUNDISHIKA
Utakapoamua kukaa chini na kufundishika Mungu atakupa double portion , utapata urejesho wa chochote ulichopoteza 
Naaman alipewa ngozi ya kitoto 
Mungu atakurejeshea ndoa yako nzuri
Utarejeshewa kibali 
Utarejeshewa biashara yako
Utarejeshewa afya yako 
Utarejeshewa watoto wako

#mwanamkenamafanikio
#soaringwomeninternational

Luphurise Lema

No comments