PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

WEKA CHUMVI KWENYE CHAKULA CHAKO

Inakuwaje unakuta chakula kinavutia kama ni rosti ya kuku imewekwa vikolombwezo kibao mchuzi mzito ndani ya bakuli nzuri ya udongo alafu unapochota na kuingiza mdomoni unakuta rosti haina chumvi..ni nini kitatokea je ule mwonekano na radha yake vitakuwa sawa mdomoni mwako.?

Kama hujaelewa vizuri chukua mshikaki uliolainishwa na tangawizi na vitunguu swahumu..ikapakwa ndimu giligilani iliki alafu ukachomwa vizuri ulipoiva ukawekwa kwenye chachandu ndipo mtu akakupitishia mdomoni mwako kama anakunyima alafu mwisho akakupa ile unaweka mdomoni unakuta hauna chumvi hata kidogo..vipi hapo utajisikiaje?

Ndivyo walivyo watu wengi ni kweli wanajua mambo ni kweli wamebobea katika mambo makubwa..wanavyeti vizuri..wanajipamba na kupendeza vizuri.lakini hivyo vyote ni kama chakula hivyo hayo yote yakikosa chumvi hayana radha kwa wahudumiwaji au wasikilizaji wako. Unapopika chakula chako usisahu chumvi maana pamoja na kwamba kwenye mwonekano wa chakula chumvi haionekani kwa macho lakini ikifika wakati wa kula chumvi inahitajika zaidi ya mwonekano.

Chumvi inaweza kuwa ni kipaji chako kidogo ulichonacho ambacho unakiongezea kwenye taaluma au kipaji chako kikubwa. Mfano katika uandishi wangu hua naweka na ushairi kidogo..katika ufundishaji wake huwa anaweka ucheshi kidogo..katika ufundishaji wake huwa anaweka (quote) msemo kidogo nk. Kama ni mcheza mpira ukiwa mfungaji mzuri basi watu watapenda upige hata chenga kidogo..na kama ni mhamasishaji ( motivational speaker) watu watataka mifano kidogo..

Cha muhimu ukumbuke chumvi ni muhimu sana lakini haipaswi kuwa nyingi yaani hapaswi kuzidi lakini pia haitakiwi kuwa ndogo au kupungua sana. Inahitajika chumvi kwa kiasi na uhitajikaji katika Chakula pikwa. Ukipatia kupika chakula ukakosea chumvi ndipo watu huweka neno lakini...tena afadhali chumvi ipungukue kuliko izidi maana Chakula kinaweza kisiliwe kabisa.

Kweli chakula chako kinavutia ila kuvutia machoni sio radha mdomoni. Weka chumvi utamu hadi kisogoni. Kiwe hotelini au kipikwe nyumbani kikikosa chumvi hakifai hasirani. Na kikizidi sana chumvi kitatupwa jalalani.

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA 

Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

No comments