PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

MALIZA SAHIHI..

Katika kuishi ndani  kuna nyakati zilizo kuu na Alama sahihi za maana Kuishi,nyakati hizo hazijawahi kuwa Rafiki wa wengi na nyakati hizo zimekuwa zikitisha kuanzia kuonekana kwake na hata utendaji wake, walio wengi hutawaliwa na nyakati hizo mpaka zikaogopeka na kuwafanya watu wengi kuamini kwamba Kufanikiwa kwa Wengi si kwa mpango wa Mungu ila kwa Njia za kishetani na utapeli yote ni kwa sababu kuwa nyakati hizo hakuna awezaye kuzishinda na KUMILIKI ushindi wa mafanikio makubwa sana.Nyakati Hizo ni VIPINDI vya Changamoto nyingi sana ambazo humshambulia mtu kiasi cha kumfanya akate tamaa na kuona yeye ni wa kuishi kawaida tu maana anafanya kila jitihada lakini Ugumu,changamoto,matatizo kuwa mengi kiasi cha kurudisha nyuma jitihada hizo..

Sikiliza yawezekana Umepata Ugonjwa ambao Madaktari na kila hospital umeambiwa unapasuliwa na ukipasuliwa nguvu za kufanya kazi zitaisha na hutafanikiwa basi unajikatia tamaa,yawezekana umepata Ajali ukaambiwa unakatwa Mkono au mguu ukaona sasa maisha yangu ndio basi,kazi yangu ya kilimo,kondakta n.k basi tena,Hapana Sio wakati wa wewe kuweka fikra,mtazamo na Nia katika kujiona umekuwaje,huwezi Fanya kazi Hapana Mbona vilema wengi hawana mikono yote,na miguu yote akiwemo NICK VUJICIC ana mafanikio makubwa ,Waliopasuliwa wengi  Leo ni wazima zaidi ya miaka  40 tokea wapasuliwe ,hawajawahi umwa tena na wamefanikiwa sana,sembuse wewe?,Hiyo huwa ni Turning point yako kwamba Kama Hujatoka Roho na hujafa ni Dhambi sana kujiona Umekufa kifikra,kimtazamo na kiutendaji ilihali u na Pumzi na akili yako I hai,Mungu hakuweka Maamuzi ya MTU katika viungo vya mwili,ila katika UBONGO(AKILI) huko ndiko kutazalisha njia mpya ya Mafanikio yako usijali vitisho unavyojijengea kwa kuwa yanapitia tatizo hilo,huko ndiko unapaswa kuweka mtazamo wa nguvu sana kwamba mpaka Tatizo lako linaisha litaisha na linakuachaje Wewe,?Likikuacha umejeruhiwa na kubaki na Kovu katika akili yako lililoandikwa SASA siwezi chochote Hakika hutokuja weza,kwa kila changamoto unayoipitia au ihangaikia kuitoa hakikisha unapokuwa unaathiriwa nayo kwa namna ya utendaji wake,Ubongo wako,Fikra zako, na mtazamo wako visiathirike kiwango cha kukuacha na kidonda au kovu Hasi, ambalo litakuwa likiamuru Maisha yako baada ya hapo,na litakuwa likiamuru maamuzi na matendo yako,Bali Baki na Kovu Chanya kwamba ndiyo nimeumia lakini haimaanishi Maisha yangu yamelimitiwa,ila kazi Fulani zimepungua zisizo sahihi kwangu na kwa kunifanikisha Mimi,sasa naanza kuifanya kazi sahihi itakayotimiza ndoto zangu,.MALIZA SAHIHI.

Umepata Hasara,umetumia nguvu nyingi kila jitihada ila mazao yamegoma,biashara imekufa hadi Mara kadhaa,umejiajiri lakini kila ukianza unaona unatumia pesa tuu faida huingizi bado mradi hujakuwa,Usimalize hiyo changamoto yako Vibaya na ikakufanya ukaamua maamuzi ya kukuathiri Maisha yote,na ukabaki kuwa MTU wa nilikuwaga.Tafadhari MALIZA SAHIHI changamoto zako na unapozimaliza umalize huku kovu likisimama kama Nyoka wa shaba,kama Tiba,na Msingi wa maamuzi sahihi ya maisha yanayoendelea.#MALIZASAHIHI.

No comments