MWANAGALIE MUNGU NA SI WANADAMU
UNAANGALIA NINI?
Siku moja mwanamke mmoja alimwendea Pastor na kumwambia; "Mchungaji wangu, sijisikii kuhudhuria ibada tena!"
*Pastor :* Kwa nini?
*Mwanamke:* Watu hawasali. Kila mtu yuko busy na simu anachati. Siji tena Kanisani.
*Pastor :* Kuna ibada sasa hivi, twende Kanisani, lakini kwanza jaza maji katika glasi hii, kisha ukifika Kanisani uzunguke mara 12 kuanzia benchi la kwanza hadi la mwisho. Hakikisha maji hayamwagiki, hata tone moja lisimwagike. Uko tayari?
Yule mwanamke alifanya kama alivyoambiwa na Pastor. Alipomaliza mzunguko wa 12, alirudi kwa Pastor kwa furaha sana, akamwambia, *"... Baba nimefaulu mtihani..."*
*Pastor :* Hongera sana. Je wakati ukizunguka umeona watu wangapi wakichati kwa simu zao?
*Mwanamke:* Sikuona mtu hata mmoja akichati, maana sikuwa naangalia watu, nguvu na akili zote niliweka katika zoezi ulilonipatia. Nilikuwa naangalia glasi ya maji tu, ili maji yasimwagike.
*Pastor :* Vema sana. Kuanzia leo, ile nguvu na akili uliyotumia kuangalia na kuchunga glasi ya maji ili yasimwagike, itumie kumwangalia Mungu wakati wa ibada, nawe hutaona mtu akichati. Ukimwangalia Mungu hutaona mapungufu ya wengine.
_Ukitaka kubadilisha wengine, badilika wewe kwanza!_
*Na sisi tumwangalie Mungu tu, naye atatubadilisha. Nasi tukibadilika, tutabadilisha wengine. Amina*
*Neema ya Mungu ituwezeshe sote.*
No comments