SITAKI HELA ITAISHA YOTE..!!
Ni kitendo ambacho kimewafanya wengi washindwe kuwekeza na kufikia mafanikio yao,walio Wengi wanatamani wawe na pesa iliyopo mfukoni sio wakose ,kuna watu wao wanaamini pesa ikiwa mfukoni ndio Anaonekana anapesa.Kuna uwekezaji unahitaji Kujikataa,Yaani ujikane Mwenyewe, unapokuwa katika hatua za uwekezaji,huhitaji kuruhusu tamaa za KUMILIKI pesa ikawa mfukoni na ukajiona unazo.YAWEZEKANA Unapata pesa hata kidogo lakini unajisikia vibaya kila ukifikiri kuiwekeza mahala Fulani kwa ajili ya Mradi Fulani,lakini kila ukipiga gharama unaona karibu zile pesa zitakuiishia nyingi halafu unabaki huna pesa,na Mwisho wake mradi wenyewe unaweza ukafa na ukawa umetumia pesa unayoipata kwa shida.
Ni kweli watu wengi wanatamani kufanikiwa sana,lakini kwanini wanaofanikiwa ni wachache sana kwa sababu watu wengi hawa wana visingizio sana,wengi hawana hiyo spirit au roho ya kuwekeza,wanajiita eti wananidhamu ya fedha,kumbe wananidhamu ya kushikilia fedha mikononi,MTU mwingine anawaza ntalala njaa nikitoa fedha yote kwenye mradi,hivyo Kufanikuwa kunakujaje kana hauko tayari kukosa fedha kabisa kwa kutafuta Fedha.?Jiulize kuna viwanda vikubwa vipi katika jamii zetu,Angalia vinamilikiwa na nani? Utakuta na MTU mmoja,hivyo Ametumia fedha kujenga
majengo makubwa ya gharama sana hapo hajaweka vifaa na mashine ambavyo ndiyo kiwanda sasa,akiweka jiulize ametumia ni nini ,jibu ni Pesa,hapo anafanya yote hayo kwa lengo la kutafuta pesa,.Lakini Wewe hata kuanza kwa level uliyonayo kuanza kutumia fedha uliyonayo ndogo kufanya kujinyima ili uwekeze kwa mradi unaoendana na kiwango cha fedha yako, ,unasema MPAKA NIPATE PESA KUBWA,(NYINGI)maana hii Itaisha,kumbe badala ya pesa kuisha Wewe ndiye unaisha.
Ili uweze kufikia Uhuru wa kifedha,lazima uweze kuithamini sana fedha ndogo unayoipata na kuipeleka katika kuwekeza kidogo ili uweze kujenga uzalishaji wa fedha nyingi,Acha kusema ntatembeaje bila pesa Mfukoni,Bali sema Ntatembeaje nikiwa mfungwa wa Taabu,umasikini na hofu ya umasikini muda wote?Acha kusema Nawezaje kuishi bila Fedha mfukoni? Sitaki Siwekezi Sahizi mpaka nipate pesa nyingi,Ndugu yangu hutakuja wekeza hata Siku moja,Mpaka utakapogundua kwamba hiyo ndogo unayoipata unaweza iwekeza na Ukapata taabu ya kukosa fedha kwa Muda kwa ajili ya maandalizi ya kupokea fedha nyingi baadae.NDIYO SPIRIT YA KUELEKEA UHURU WA KIFEDHA.
#TETE,#MotivationalSpeaker.
Sadick Tete, 0762490145:sadicktete24@gmail. com
No comments