PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

FIKRA ZAKO ZIMEUNGANISHWAJE?(Thought connection.)




Jumanne ya Leo tar 13/03/2018,Natamani nikutafakarishe kuwa,kadri unavyoishi na enenda ndivyo vitu vya aina ya maisha unayoishi vinakuwa connected kwako,(vina unganishwa) ,Kadri unavyofikiria sana,ndivyo macho yako yanajikita kuyaona Yale tuu yaliyotawala fikra zako,hata kama yangejitokeza Mengi njiani,Hutayaona Yale yasiyosumbua fikra,...Mfano,kama fikra zako zipo ktk uhitaji wa Mwanamke/Mwanaume,Au fikra zako zikitawaliwa na wanawake/wanaume,Njiani mwako utajikuta unachunguza na kumfuatilia kila MWANAMKE/Mwanaume utakaye Muona akipita machoni pako,kama unawaza mpira kila utakapo pita ukiona watu wengi na sauti za mipira utasimama na kufuatilia,ukijikita ktk kukagua makosa ya watu,njiani mwako utakuwa MTU wa kukosoa watu na maisha yao n.k

Ukitawaliwa na uhitaji wa FURSA, njiani mwako utajikuta kila unachokiona kinameng'enywa Fikrani haraka  na kufanywa Fursa au laah,Ukiunganishwa na Jicho LA Fursa hakika hutoona jambo bila kutafakari kifursa,Yawezekana njia yako unayopita kila wakati INA maduka 10,lakini hujui kitu gani wanakosa wote hao wengi Maduka,,Unatembea mashambani Mara kwa Mara,bado hujagundua  zao gani halilimwi sana kibiashara na wakulima wote, Mfano MCHICHA BANGI,MAJIMBI,MIHOGO Mikoani,n.k Lazima kila hatua ya maisha yako I,iambatane na SULUHU ya changamoto yako kiuchumi,Fikra zako Muda wote kuanzia sasa ziwe connected,ziunganishwe na FURSA,Macho ya kifursa,Na mtazamo wa utatuzi wa fikra binafsi,,na ukiiona fanyia utafiti Mara moja,na uchukue hatua sitahiki kuelekea Fursa hiyo,,,Sijui wewe umenganishwa na nini? Unaona nini njiani mwako,unajihusishaje ktk kutembea kwako sehemu mbali mbali,unatumiaje mwendo wako na njia yako,kuifanyisha akili kazi, inasaga vitu gani akili yako unapokuwa unatembea njiani mwako, Je ni wanaume au wanawake,mapenzi,Fursa,Kukagua makosa ya watu,malalamiko ya ndoa?au ni nini zaidi?

Mimi nimetembea bustani nikaona Fursa kupitia majani haya,ya zao LA Majimbi,#Beconnectedtoooportunity.
#JiunganishenaFursa.,Je,Tafakari,ni kwa kiasi gani Zao LA Majimbi linalimwa kwenu?na soko lake huko kwenu,pamoja na mboga majani,mchicha bhangi na mihogo kwa wale wa mikoani,hiyo so Fursa kwenu pia?..


#TETE,#MotivationaSpeaker,Sadicktete24@gmail, 0762490145.


No comments