MUNGU ANAHITAJI MAWASILIANO NA SISI.
Msimamizi wa ujenzi alikuwa anamwita mjenzi chini ya jengo yeye akiwa ghorofa ya 16. Lakini kwa sababu ya kelele za nje, mjenzi pale chini hakusikia sauti hiyo.
Ili kumfanya mjenzi ashtuke, msimamizi alirusha noti ya sh elf 5, kutoka juu na ikaangukia alipo mjenzi yule. Mjenzi aliokota, akaweka mfukoni na kuendelea na shughuli zake.
Msimamizi akarusha tena noti ya elf 10 kwa mjenzi yule. Kwa nia ya kumshtua ili wawasiliane, wakati huu pia mjenzi aliokota ile elf 10, akaiweka mfukoni na kuendelea na shughuli zake.
Sasa msimamizi akaamua kuchukua kajiwe kadogo na akarusha kakampata mjenzi. Safari hii, kwa sababu kale ka jiwe kalimuumiza, aliangalia juu ajue kalipotoka, Ndipo msimamizi alipopata nafasi ya kuwasiiana.
Hebu tafakari kwa muda. Mungu anataka mawasiliano nasi, lakini tuko busy na shughuli zetu za dunia hii.
Anatupa zawadi/ baraka kubwa na ndogo tunazichukua na kuzifurahia bila hata kujua zinatoka kwake, bila hata kushukuru. Na mara nyingi tukijisifu kuwa TUMEBAHATIKA.
Lakini pale tunapo rushiwa kajiwe kadogo, ambacho tunaita (MATATIZO), ndipo tunamkumbuka Mungu.
Hapo ndipo tunapoomba/sali na kuwasiliana na Mungu.
Mungu anatupatia vyote na kutusamehe dhambi, sisi tunapokea na kusahau, tubadilike, Mungu hafurahii.
Tusisubiri turushiwe mawe, wakati wote tumkumbuke na kumsifu Mungu.
Tufanye kumuomba,kumshukuru na kumsifu Mungu iwe sehemu ya maisha ya kila siku...ubarikiwe
No comments