JIKONI KWA MAFANIKIO KUKOJE?
JIKONI KWA MAFANIKIO KUKOJE?
MAFANIKIO katika Maisha ni mchakato mrefu sana na mchakato huu,umewafanya wengi kutoelewa kipi cha kuvutiwa nacho kutoka kwa waliofanikiwa,sikia watu wengi wameamini mafanikio ni Yale yanayoonekana kama vile Nyumba nzuuri,Magari,wapenzi na wanandoa kushinda wote,kutembea wote kwa kufanana na msonekano wa upendo kwao ndiyo hayo walio wengi tunayatamani tukiona kwa wengine,tukiona Biashara nzuuri na makampuni yanaendelea n.k tunona na sisi tungekuwa hivyo,au tuwe hivyo,...
Sikiliza Mafanikio yoyote yanaanzia jikoni huko jikoni kukoje? Ndani yako,maandalizi yakoje? Hayo yanayoonekana nje,Nyumba,Magari,mapenzi mvuto kwa wanandoa,Biashara na makampuni ni MATOKEO ya mapishi yanayofanyika Jikoni,umeweka mawazo(Ideas) gani nafsini kwako,umewekeza nini ni mbegu gani Kwenye Nafsi yako,na unafikiri hayo mawazo,Ideas zitakuja toa matokeo gani nje,Mafanikio ni Mchakato unaoanzia Jikoni (Ndani) yako na jinsi unavyopika(Mapishi ya mawazo) hayo,unakuta MTU lile analolipanga,analolitaka, analolipenda Halifanyi,ila lile asilolitaka ndilo anafanya, yaani kile mwili wako unataka unafanya haraka sana,mpira,mapenzi,nguo, kujionesha,kujifanya umefanikiwa na una Maisha safi,unafanya haraka sana,ila Yale Roho yako inataka kama kuwa na nidhamu ya pesa,mkimya,mtendaji na kujituma,kuvumilia changamoto,kufeli na kuanza tena,kujaribu kwa maamuzi binafsi,kujitoa ipasavyo kwa ndoa yako, Biashara na kazi yako,kujali na kuheshimu muda hutaki,nidhamu ya mwelekeo na maamuzi hufanyi ila vile usivyovipenda unavifanya haraka,Jikoni hakuendani na vyakula vilivyopikwa,
Jiko lina maandari ya vyakula hivi,ila vinavyoliwa vya mgahawani,mbona sio wewe unaepika vyakula unavyokula? Ni huwezi kufanikiwa kama utaendeshwa na mwili,ukiendeshwa na mwili wako,mfano ukisikia sana maneno wanayokusemea,ukitamani kila jicho linachoona,kila harufu unusayo tamuu,ukipenda kula vitamuu tuu,ukipenda kusifiwa tuu,ukipenda kubadili nguo,na viatu,n.k ukipenda kila mwanaume/mwanamke awe wako,Sahau kufanikiwa ndugu...Haya mambo ni Mchakato unaoanzia Ndani kuja nje,sio nje kwenda ndani.....LAZIMA UJUE JIKONI KWAKO KUNAKOPIKA MAFANIKIO KUKOJE? NA KUNAPIKA MAPISHI GANI?
#TETE,#MotivationalSpeaker,Sad icktete24@gmail.com
No comments