MAISHA YANGU NA KAPU LA NDIZI
Huku ndiko niliko tokea,
Leo nimekutana na Makapu ya wamama wauza Magenge nikakumbuka nilivyokuwa mdogo Nilibeba kichwani kutoka soko kuu Hapa Dodoma ambapo Leo hii ni Nyerere Square, baadae lilihamia Majengo;
sasa kipindi hicho mtoto wa Kiume kubeba kapu kichwani ilikuwa sio jambo rahisi, nilichekwa sana na wenzangu ila nilipambana nao wakati Mwingine Mpaka kupigana.
Mnisamehe niliowapiga kwa kunicheka ila sikuachwa na wazazi sikuwaambia kuwa nachekwa kwakubeba makapu nilijuwa ndio Maisha Yetu. Leo hii sioni aibu kufanya kazi yeyote hii nikutokana na misingi kutoka kwa wazazi hawakuchagua kazi kwa watoto wao iwe kulima ama kupika hawakuchagua Jinsia.
Ujumbe kwa wazazi wote na Walezi; Tuwashirikishe watoto kazi tuzifanyazo nakuwapa Ujuzi bila kuona aibu ili mradi ujuzi au kazi haivunji Sheria za nchi Wala kutweza utu wa Mtu.
Nakuhakikishia huu ndio Urithi Usiogombewa na Ndugu, kumbuka watoto wanajifunza asilimia 75% kwa kuona na sio unayowambia na kuwaonya wakiona unatabia mbaya wataiga wakiona Mazuri wataiga.
Najuwa likizo zimeanza pamoja na Shule nzuri tunazowalipia watoto wetu; kipindi cha likizo ndicho kipindi watoto wanatakiwa wajifunze kazi za nyumbani. Hakikisha wanashiriki kama ni mkulima,mfanyabiashara watoto wanajifunza unachofanya kitakuja kuwasaidia siku za Usoni uwepo hai ama Haupo, weka kitu kwenye maisha yao kitawafanya wakukumbuke.
Mimi nimeona kwa wazazi Mama alikuwa Mfanyabiashara wa Mkaa na Genge, Baba alikuwa Mfanyakazi ameajiriwa Serikalini ila alikuwa Mkulima wa Mahindi, pia Bustani za Mbogamboga bila kusahau alikuwa akishona kwa Cherehani alifanya hayo baada yakutoka kazini saa tisa na Nusu.
Kwa Sasa baba kastaafu yeye na Mama ila bado niwafanyabiashara na wakulima, hakika nawashukuru sana wazazi wangu Mungu awabariki.
Wale mlioishi Area C Dodoma kata ya kiwanja Cha ndege miaka ya 1988 kuja juu mtasadifu haya niyasemayo.
Elirehema Msuya
#kazinaututunasongambele #UfalmeTV
No comments