PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

NAMNA UNNAVYOONGEA NA MWANAUME INAWEZA KUWA NDIYO SABABU HAKUSIKILIZI



Wakati mwingine inawezekana unagombana na mume wako kwakua tu hamuongei lugha moja, hakuna mawasiliano. Kiasili mwanaume ameumbwa kujiona kua yuko juu na hakuna mwanaume anayependa kukaliwa juu na mwanamke.

Kwamba mkewe amuambie nini cha kufanya na kumpangia. Ukishaanza kumpangia vitu mwanaume anaanza kujisikia vibaya na anaona unamtawala na anaweza kupinga tu si kwasababu anataka bali kwakua unamuamrisha.

Labda niwape mfano mmoja, wanawake wengi hulalamika kua waume zao huchelewa kurejea nyumbani, na mume akifika nyumbani mke huanza kulalamika na kununa. 

Wengine huenda mbali zaidi na kuanza kusema kua “Sitaki uwe unanirudia usiku! Ulale huko huko…” na maneno mengine kama hayo.

Hakuna namna ambavyo utamfanya mwanaume wako kuwahi kurudi kwa kauli hizo. Kwanini umpangie? Ataanza kuwaza hivi huyu ndiyo nimemuoa au kanioa?

Akiongea na marafiki zake watamshangaa, unaendeshwaje endeshwaje na mwanamke? Ndiyo hata ndugu na Mama yake atamshangaa.

Nikitu kizuri kuwahi kurudi nyumbani na yeye anajua lakini ukishaanza kumpangia muda wa kurudi basi jua mtagombana tu.

Lakini unatakiwa kufanya nini, hembu amua kua mwanamke na muache awe mwanaume, kua mnyenyekevu na muambie kistaarabu.

“Mume wangu naomba basi leo uwahi kidogo kurudi… kuna chakula nataka nikupikie sitaki tule kikiwa kimepoa..” Unamaliza ukitabasamu, hujalazimisha umeomba.

Atakuahidi nitajitahidi ili asikukwaze kwakua ulimuomba na hukumuamrisha, hatataka kukukomoa kwani huna cha kukomolewa.

Anaweza kuwahi kurudi au kwakua kashazoea kuchelewa basi atachelewa, atakuta chakula kilichopoa na atajisikia vibaya hata kama hatasema.

Wewe wala usikasirike, kaa baada ya week muombe tena kuwahi ili mle pamoja, baada ya muda ataanza kuona umuhimu wa kuwhai kula na mkewe.

Kwamba atajua kua suala la kula pamoja kwako ni muhimu. Sasa angalia wewe ingawa lengo lako ni ili awahi kufika nyumbani lakini unamuambia kuhusu chakula.

Sasa anajua kua humpangii muda wa kurudi lakini kwakua unampenda basi unataka mle pamoja. Huu ni upendo wakati kulalamika anachelewa ni amri ya kumtaka kuwahi.

Ndoa ndiyo ilivyo, hampaswi kushindana bali wote kufanya mambo na kuwa katika ukurasa mmoja. Hupungikiwi kitu ukisema “Naomba” lakini unaongeza upendo kati yenu.

Flaviana Lyimo

No comments