PAMBAZUKO JIPYA

Breaking News

UKIWA KAMA JANA UNAFELI.....


Kitu pekee cha kujifunza na kujikumbusha Leo ni kwamba,Ukiona umeianza siku mpya na Fikra za Jana,au bila fikra mpya,bila upya wowote wa Fikra,mtazamo,Nia na Maono(VISION), UJUE UMEANZA KUFELI NA KUSHUKA CHINI KWA MWENDO MBAYA.,Watu wengi wanaingia kazini kwao kwa sababu tu ndiko huwa anaenda kila siku,kwa sababu tuu ni lazima aende ,hivyo Anakuwa anaenda kawaida tu kama alivyoenda juzi,na Jana,akifikiri sana tofauti anakumbuka Jana alifanya kazi gani na Leo anaenda kufanya ipi.,Kuna watu wakati wanaanza kazi, biashara,au ujasiriamali flani walikuwa watu wa Kupenda kula Maarifa kwa kusoma vitabu kila siku,kusoma post za hamasa kila siku,walikuwa wana mawazo mapya na ubunifu kila wakati,asubuhi hadi jioni haikufika bila wao kuwa na Fikra za nguvu na mitizamo mipya na chanya sana,ila baada ya muda mfupi eti wako busy sana kuliko maarifa,wako busy sana hawawezi kusoma,wametingwa sana kuliko ujuzi,wametingwa sana kuliko Fikra chanya na mitizamo chanya iliyopo katika Vitabu,video na Post mbalimbali,..na ndio siri ya wengi wao kuishi kawaida,ndio siri ya wengi kuishi na kuanza kazi na kumaliza kama Jana...

Na ukifikia kiwango cha kutoona na kujiona Tofauti kati ya Jana na Leo, asubuhi na mchana na jioni katika kazi yako, biashara yako,na ujasiriamali wako,UJUE UMESHAANZA SAFARI YA KUFELI SIO KUFANIKIWA TENA,ila utastuka baadae sana utakapoanza kutafuta uchawi badala ya mchawi,..Hakuna siku MTU anatakiwa aishi kama Jana au muda uliopita ni mwiko,lazima uwe mpya kila wakati,lazime ulishe Ubongo wako na ubongo utoe athari chanya kwa matendo ya nje,ndio SIRI YA WANAOFANIKIWA SANA MPAKA LEO.

Ukianza au kumaliza kama unavyomaliza Jana n.k #UNAFELI SANA.

No comments