NI KILA FURSA YAKO!?
Unajua watu wamekuwa waoga sana wa maisha, na uhitaji wa mafanikio umekosa Discipline yaani Nidhamu,ni kweli Matitizo ni Fursa,Na katika nchi yetu hii Kuna matatizo/Changamoto nyingi sana,ambazo Leo hii zimegeuzwa kuwa FURSA,na kujikuta Tanzania kuwa nchi ya FURSA nyingi sana za kimafanikio,Lakini pamoja na FURSA nyingi zilizopo bado watu hawafanikiwi kama walivyokusudiwa na kuingia katika FURSA hizo,Nini sababu ya kutofanikiwa kwao,TAMAA,NA ULAFI,Tumefikia mahali kila FURSA tunayoisikia ni ya kimafanikio tunataka tuifanye,au tujiunge nayo,tunataka itufanikishe,Ndiyo maana Kufanikiwa kumeendelea kuonekana ni kwa baadhi ya watu flani tu siku zote,Ukusikia Ajira umo,ukusikia part time Fulani ina kamshara kazuri unataka uwemo,ukusikia biashara ya mazao umo,ukusikia mgahawa umo,Ukisikia NETWORKING BUSINESS,(biashara ya mtandao Ndiyo kabisa,huku watu wengi wanalia na kuona hiyo biashara ni ya kihuni na kishenzi, Mara DM marketing,Mara TREVO,Mara Forever Living product, Mara QNET,ukusikia kilimo unataka,ukusikia Ufugaji kuku,sungura n.k unataka n.k sasa watu wengi wameshindwa kuelewa hili,.
Si kila FURSA ni yako,lakini swala sio umeiona FURSA basi unataka kufanya,Angalia Ndani yako,una Passion,Una mguso na msukumo na Hamu ya kufanya hiyo?sio unaingia tuu kisa umeambiwa Kuna faida,na mafanikio, Si kweli,Eti umeambiwa utafanya kama part time huku ukuendelea na kazi zako basi wewe sawa,Ndugu Maisha hayahitaji maamuzi ya kurukaruka hivyo,hayahitaji uwe juu,juu tu na Maamuzi yako,Maisha yanataka nidhamu,maamuzi sahihi sio maamuzi tu,Maisha hayahitaji Tamaa za kufanikiwa yanahitaji Uhitaji wa kufanikiwa,Yawezekana Umeambiwa kazi unayofanya Watu huwa wanafanikiwa Uzeeni,na wachache,Mwambie Mimi ntakuwa wa kwanza kijana,Maana unaifanya,kwa sababu wewe ndiye ulitakiwa uifanye,Acha kubabaika na FURSA babaika na Wewe Unataka nini,babaika na wewe Unaona nini, Wewe ni nani Na FURSA unaionaje,.
Huwezi Leo unaianza FURSA hii miezi mitatu,mwaka umeacha umeanza uliyoisikia mpya,cha kujiuliza ni,Ni kama hao wanaofanya Wameacha kazi zao walizokuwa wanafanya wakaamua kujiunga na hizi,wewe utawekezaje Muda kidogo? Kama ni kazi inayofanikisha haraka,kwanini inategemea waliofanikiwa awali,kwani hao waliofanikiwa,walifanikiwa kwa kazi ipi? Sikiliza haihitaji kuamini kila FURSA ni yako, ila kila FURSA inafanikisha,sio kila FURSA kwa sababu ni FURSA itakufanikisha,Hapana FURSA nyingine ni za wengine,na wewe una zako,Utazijuaje,Uwezo na nguvu ya Mguso na msukumo ndani yako(passion),Nguvu ya kuhitaji ndani yako,Lazima ujue kutofautisha kati Ya KUTAKA,KUTAMANI NA KUHITAJI,Nguvu ya kuisikiliza ni JE,kiasi gani Unahitaji kufanya hicho kitu,au unataka kufanya Nakumfurahisha Aliyekualika,na kukuonesha FURSA hiyo,sikiliza,USIMFURAHISHE MTU kwenye Maisha yako, Bali Fanya maisha yako ili wao wafurahie maisha yao kupitia wewe, kuwa na NIDHAMU ya kujua nini unataka na kuhitaji,.Kuwa na Mwelekeo,ukikosa Mwelekeo,kila upepo utakaokukuta njiani utakubeba,kila atayekukuta akikuomba nisindikize utaenda,Maana hujui unataka nini na unaenda wapi?
#TETE,#MotivationalSpeaker,Sad icktete24@gmail.com
0762490145.
No comments