LEO NI LEO.....!!!YES
Maisha ni mapito na kila tunalolifanya na linalotutokea ni kwa muda tuu,kama vile ukiwa umetulia halafu ukasikia kichwa kinagonga kwa dk kadhaa,na Maisha yetu yanatokea kwa siku moja tuu, yaani Leo. Kila hali inayokutokea Maishani sio ya kudumu ni mapito, kwa kuwa hata wewe ni mapito maana hukuwahi kuwepo hapo kabla,ukaja kuwepo na siku uliyopo ni LEO na SASA, sio Jana wala kesho,Pia HUTAKUWEPO TENA, maana unapita na unatoweka,.Hivyo usifikiri ugumu unaoupitia maishani mwako,changamoto hiyo itatudumu hapana,Itapita tuu.
Kumbuka,Usije idharau Leo kwa kujua kesho IPO,ili Ufanikiwe siku zote ktk Maisha yako,ISHI LEO ipasavyo,izingatie Leo,Hilo wazo lako lifanye Leo,Kwa kuwa unaishi Leo,na Mafanikio yako yanapatikana Leo na sasa,Uzima wako na Afya yako iko hivyo SASA,iko vizuri sasa,wewe ni MZIMA sasa,na Leo,hapo ndipo pa kuishi ipasavyo,kujituma vilivyo na kupambana vilivyo,Huo Uzima nao unapita,ukipita Uzima utakuja ugonjwa au kifo,Usiidharau LEO NA SASA kwa kujua kesho IPO,Maisha ni mapito,wewe na kila hali unayoipitia ni Mapito..unapopitia kipindi hiki,na kipande hiki cha Maisha ukiwa ulivyo,mzima kitendee haki kipande hiki.,Maana kuna kipindi kinakuja kupita baada ya hiki kitakutendea HAKI.Usiionee HURUMA Leo na sasa yako. Maana kipindi na kipande kijacho cha changamoto, ugumu,ugonjwa,au kifo,Hakitakuonea HURUMA KABISA.
#Kila kitu ni LEO na SASA, Ishi Leo,Fanya Leo,Fanikiwa LEO, na Kuwa unayetaka kuwa LEO.Kama sasa na LEO unapitia hali ngumu na mbaya kumbuka,UNAPITIA,utapita hapo na hali yako nzuri na USHINDI Unakuja,...
#TETE,#MotivationalSpeaker,Sad icktete24@gmail.com, 0762490145.
No comments